SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA VETA WILAYA ZOTE

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe profesa Adolf Mkenda amesema serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika Wilaya 64 nchini. Waziri Mkenda amesema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika kipindi…

Read More

Kiungo Singida agomea mamilioni | Mwanaspoti

SINGIDA Black Stars imeanza harakati za mapema za kumuongeza mkataba mpya, kiungo Morice Chukwu, huku Mnigeria huyo akiwagomea mabosi hao, licha ya kuahidiwa donge nono. Chukwu alisaini mkataba wa miaka mitatu na timu hiyo, huku akiwa amezitumikia klabu tatu tofauti hadi sasa kote alikwenda kwa mkopo. Mnigeria huyo alianzia Singida Black Stars, kisha akapelekwa Singida…

Read More

Mchakato kodi ya majengo usajili waanza upya

Dar es Salaam. Baada ya miaka minne ya ukusanyaji wa kodi ya majengo kupitia mfumo wa ununuzi wa umeme kwa kutumia mashine za Luku, inaripotiwa kuwa Serikali ipo katika hatua za mwisho za kubadilisha mfumo huo. Kuanzia mwaka ujao wa fedha, kodi hiyo inatarajiwa kukusanywa moja kwa moja kupitia halmashauri. Mchakato wa maandalizi tayari umeanza…

Read More

NBAA na BOT Wasisitiza Uwajibikaji wa Kifedha

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT), imeandaa semina ya pamoja uliyowakutanisha wataalamu wa uhasibu, wakaguzi wa hesabu na wadau wa sekta ya fedha kutoka ndani na nje ya nchi. Akifungua rasmi semina hiyo iliofanyika jijini Arusha, Gavana wa BOT, Emmanuel Tutuba, alisisitiza…

Read More

Janabi aingia rasmi WHO, aahidi mageuzi ya afya

Dar es Salaam. Profesa Mohamed Janabi, ameapishwa rasmi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, huku akiahidi kuboresha afya za watu wa Afrika. Profesa Janabi amekula kiapo hicho leo, Mei 28, 2025 ikiwa ni siku 11 tangu alipochaguliwa Mei 18, 2025 wakati wa kikao maalumu cha ana kwa ana cha kamati…

Read More

Maadhimisho ya wakulima wa NOURISH yafikia tamati Babati

Na Mwandishi Wetu, Manyara MAADHIMISHO ya wakulima wa NOURISH yaliochukua wiki nne kwa nyakati tofauti katika halmashauri za wilaya 10 Tanzania, yamefikia tamati katika Wilaya Babati na kufikia wakulima maelfu kupitia elimu ya kilimo chenye tija na lishe bora. Wilaya ya Babati imehitimisha kilele cha maadhimisho hayo ambayo yalianza mnamo mwishoni mwa mwezi wa nne…

Read More

Pina mwamba aliyeandika rekodi mpya Zanzibar

UNGUJA: STRAIKA wa Mlandege na nyota wa timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, Abdallah Idd ‘Pina’ ameweka rekodi Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) wakati msimu ukiwa ukingoni. Pina aliyekosa mechi saba kati ya 27 ilizocheza timu hiyo anamiliki mabao 19, amekuwa gumzo kwa kufunga hat trick mbili katika mechi moja ya ligi shidi ya Tekeleza…

Read More