Hiki ndio kitakachomaliza urasimu, migogoro ya ardhi Zanzibar
Unguja. Wakati Zanzibar ikizindua kwa mara ya kwanza kanuni za uhaulishaji wa ardhi, hatua hiyo inatajwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza migogoro ya ardhi na kuondoa urasimu uliokuwa ukifanywa na watendaji. Pamoja na hayo, pia itapunguza muda na mchakato mrefu kwa wananchi kwasababu shughuli zote za uhaulishaji, ukodishwaji na kutoa hati zitafanywa sehemu moja tena…