Polisi Mbeya yakanusha kuhusika tukio la kushambuliwa Mdude
Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa askari wake wanahusika katika tukio la kuvamiwa na kupigwa kwa kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni mwanaharakati, Mdude Nyagali. Kwa mujibu wa Jeshi hilo, taarifa hizo siyo za kweli na zinalenga kupotosha umma kuhusu…