Makada Chadema walioishtaki INEC watoa kauli

Dar es Salaam. Mwaka mmoja baada ya kuundwa kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), makada watatu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamefungua shauri kupinga sheria hiyo. INEC imeanzishwa mwaka 2024 chini ya Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), namba 2 ya mwaka 2024. Sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge Februari 2,…

Read More

Kweleakwelea wazua vilio kwa wakulima Mbarali, watalaamu waingilia kati

Mbeya. Wakati wakulima wa zao la mpunga wilayani Mbarali, mkoani Mbeya, wakijiandaa kwa msimu wa mavuno, taharuki imetanda kufuatia mashamba kuvamiwa na ndege aina ya kweleakwelea, hali inayowaweka wakulima katika mashaka na kuwafanya waombe msaada wa haraka kutoka serikalini ili kunusuru mazao yao. Ndege hao wanadaiwa kuanza kuvamia mashamba hasa katika kipindi cha kuelekea mavuno,…

Read More

Wanaojitolea katika taasisi za umma hii hapa neema

Dodoma. Serikali imetangaza kuanza rasmi utekelezaji wa mwongozo wa kuwatambua na kutoa kipaumbele kwa wanaojitolea katika kazi mbalimbali, hasa pindi zinapotokea nafasi za ajira. Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Deus Sangu, aliliambia Bunge leo, Ijumaa Mei 2, 2025, kwamba mwongozo huo utaanza kutumika rasmi kuanzia Julai Mosi, 2025. Naibu Waziri alikuwa akijibu swali…

Read More

Benki ya NBC Yashiriki Maadhimisho Mei Mosi Singida, Yasisitiza Dhamira Yake Kuwafikia Wafanyakazi Zaidi.

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na mamilioni ya wafanyakazi kote nchini na duniani kwa ujumla kusherekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, MEI Mosi ambayo kitaifa yamefanyika kwenye Viwanja vya Bombadia Mkoani Singida, yakiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Maadhimisho hayo yaliyohusisha wafanyakazi na viongozi wengine waandamizi akiwemo Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,…

Read More

Kayombo atembelea kambi ya wanamichezo wa TRA

Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Richard Kayombo amesema kuwa ushiriki wa wanamichezo kutoka TRA katika  michezo ya aina mbalimbali katika michezo ya Mei Mosi unalenga kusambaza ujumbe wa ulipaji kodi pamoja na kuhamasisha suala zima la kutoa na kudai risiti za kieletroniki za EFD. Mkurugenzi Kayombo…

Read More

TARURA KUANZA KUTANGAZA ZABUNI ZA MWAKA 2025/2026

📌Barabara zenye changamoto kufikiwa 📌Zipo barabara zenye kipaumbele kwa jamii. Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amewaagiza Mameneja wa Mikoa nchi nzima kuanza kutangaza zabuni za mwaka wa fedha 2025/26. Mhandisi Seff ameyasema hayo jana alipotembelea ofisi ya Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida pamoja na kuzungumza…

Read More

Sintofahamu Mdude kukamatwa, polisi yasema wanafuatilia

Mbeya. Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mbeya, Hamad Mbeyale, amelitaka Jeshi la Polisi kueleza iwapo linamshikilia mwanaharakati Mdude Nyagali na kutaja kosa wanalomtuhumu, pia amesimulia namna alivyokamatwa. Kwa mujibu wa Mbeyale, baada ya kufika nyumbani kwa Mdude, majirani walieleza kuwa watu waliovunja mlango, kumshambulia kwa kipigo na baadaye kuondoka naye,…

Read More

Muuguzi auawa kwa kuchomwa kisu, muuaji adaiwa kujinyonga

Bunda. Muuguzi wa Zahanati ya Kijiji cha Malembeka kilichopo wilayani Bunda, Mkoa wa Mara, Zawadi Kazi (31) amefariki dunia baada ya kuchomwa na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake na mtu anayedhaniwa kuwa ni mpenzi wake kwa kile kinachelezwa ni ugomvi wa kimapenzi. Baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa huyo alikimbilia kusikojulikana  hata hivyo mwili…

Read More