Tanzania yaongeza kasi utafiti wa mafuta maeneo mawili
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu wa Petroli (Pura), Charles Sangweni amesema wameongeza kasi ya utafiti wa kina katika maeneo ambayo wanaamini kuwapo kwa viashiria vya mafuta nchini, ikiwemo Eyasi-Wembele na Ziwa Tanganyika. Wakati hilo likifanyika, pia, Pura imeita wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya gesi na mafuta kuchangamkia fursa iliyopo…