Rais Samia amteua Badru bosi mpya Ngorongoro, Dk Doriye aliwa kichwa
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili akiwemo Abdul-Razak Badru aliyeteuliwa kuwa Kamishna wa Uhifadhi katika Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), akichukua nafasi ya Dk Elirehema Doriye ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Badru anachukua nafasi hiyo baada ya kuhudumu kama Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii…