Watumishi halmashauri ya Mji Njombe wafanyiwa maombi
Njombe. Watumishi wa halmashauri ya Mji Njombe wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa ili kuleta matokeo chanya kwa halmashauri na wananchi wanaohudumiwa. Wito huo umetolewa leo Mei 31, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Kuruthum Sadick wakati wa dua ya kuwaombea watumishi wa halmashauri hiyo iliyofanyika huko wilayani Njombe. Amesema wanapoelekea…