Mbeya City yaanza usajili Ligi Kuu Bara, Malale naye ndani

Timu ya Mbeya City imesema wakati ikiendelea na usajili, lakini upande wa benchi la ufundi imeshamalizana na Kocha Mkuu, huku ikikiri wapo wachezaji watakaoachwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo matakwa yao. Pia imesema baada ya kufanikiwa kutimiza malengo ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao, itaandaa sherehe Mei 31 kupongezana kutimiza malengo. Akizungumza leo Jumapili Mei…

Read More

Kinachowasibu wazazi malezi bora kwa watoto

Katika ulimwengu wa kisasa unaoendeshwa na maendeleo ya teknolojia na utandawazi, wazazi wengi wanakumbana na changamoto zinazobadilisha mbinu zao za malezi. Hali hii inawafanya baadhi kuonekana kama wameacha majukumu yao ya msingi. Ni muhimu basi kuchunguza chanzo cha hali hii na nini kifanyike ili kukabiliana nayo. Hivi karibuni nikiwa kwenye mihangaiko yangu nilikuta na Sabina…

Read More

Familia ya Mchungaji aliyetekwa yasema inamwachia Mungu

Arusha. Familia ya Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya Kristo lililopo Mtaa wa FFU, Kata ya Muriet mkoani Arusha, Steven Jacob, aliyekuwa ametekwa na watu wasiojulikana na baadaye kuokolewa na walinzi wa mashamba ya ngano mkoani Kilimanjaro, imesema inamuachia Mungu kwa kile kilichotokea kwa ndugu yao. Mchungaji Steven alitekwa na watu wasiojulikana alipotoka nyumbani kwake…

Read More

Watatu waachiwa huru usafirishaji gramu 997.91 za heroini

Arusha. Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, imewaachia huru washtakiwa watatu walioshtakiwa kwa kosa la kusafirisha gramu 997.91 za dawa za kulevya aina ya heroini. Hukumu iliyowaachia huru washtakiwa hao imetolewa Mei 23, 2025 na Jaji Sedekia Kisanya aliyesema upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha shitaka hilo pasipo kuacha shaka. Walioachiwa huru ni Mohamed…

Read More

Wizi mpya Kariakoo unavyowatisha wafanyabiashara, wananchi

Dar es Salaam. Mbinu mpya ya uhalifu imezuka katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa wahalifu kutumia ugomvi bandia kuwaibia wafanyabiashara na watu wengine wanaofika eneo hilo la kibiashara. Mbinu hiyo ya kihalifu inatekelezwa na makundi ya vijana, ambapo mmojawapo humsogelea mtu ambaye ni mgeni wa mitaa husika kisha kuanza kumtuhumu kwa sauti,…

Read More

Mbeki: Tatizo sio sera, shida watekelezaji

Dar es Salaam. Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki alisema Afrika haikabiliwi na changamoto ya sera bora, bali inakumbwa na tatizo la ombwe la watekelezaji wa sera hizo kwa manufaa ya watu wake. Katika hoja yake hiyo, alisema kuna umuhimu kwa bara hilo, kuzalisha rasilimali watu itakayomudu utekelezaji wa sera hizo na hatimaye Afrika…

Read More

Thadeo Lwanga azifuata Simba, Yanga CAF

KIUNGO wa zamani wa Simba, Thadeo Lwanga, 31, amebeba ubingwa wa Ligi Kuu Rwanda akiwa na APR, leo Jumamosi baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rwamagana City na kufikisha pointi 64. Lwanga ambaye aliichezea Simba kwa misimu miwili kati ya mwaka 2020 hadi 2022, hili linakuwa ni taji lake la pili la…

Read More

Ukiona haya, jua uhusiano, ndoa yako feki

Watu wengi sana wako kwenye uhusiano feki bila kujijua. Yumkini kwa sababu ya kiu ya kupendwa na kupenda, kiu ya kujisikia kuwa niko kwenye mapenzi bila kujali uhalisia wa huyo mwenzake. Lakini pia kukurupuka au kwenda pupa katika kufanya uamuzi unaohusu uhusiano, kunawagharimu walio wengi. Uhusiano wa kweli sio jambo rahisi sana maana unahitaji jitihada…

Read More

Joto Zanzibar laitesa Berkane | Mwanaspoti

WAKATI  kikosi cha RS Berkane kutoka Morocco kikijipanga kuivaa Simba SC katika fainali ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika, hali ya hewa ya Zanzibar inaonekana kuwatesa Waarabu hao. Kwa siku kadhaa tangu kuwasili kwao Zanzibar usiku wa Alhamisi wiki hii, hali ya hewa inayofikia nyuzi joto zaidi ya 32°C mchana imekuwa kero kwa kikosi…

Read More