Bima ya lazima kwa wageni yazalisha Sh16 bilioni Zanzibar
Unguja. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema imekusanya Sh16.177 bilioni kwa miezi mitano kupitia malipo ya bima ya lazima ya Dola za Marekani 44 (Sh118,404) kwa kila mgeni anayeingia Zanzibar. SMZ ilianzisha sera maalumu ya kutoza wageni wanaoingia nchini,na utekelezaji wake ulianza rasmi Oktoba mosi, 2024. Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi, Mei 22, 2025 na…