Wadau watoa neno vipaumbele vya elimu 2025/26
Mwanza. Wakati Bunge lilipitisha bajeti ya elimu kwa mwaka 2025/26, wachambuzi na wadau wa elimu wameelezea hisia zao kuhusu vipaumbele vilivyowekwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Bajeti hiyo ya Sh2.4 iliwasilishwa bungeni Mei 12, 2025 na Waziri Elimu, Profesa Adolf Mkenda kisha, Bunge kuipitisha, ikiwa imeongezeka kwa asilimia 23.8 sawa na Sh0.469 trilioni…