WAZIRI AWESO ATAKA WANANCHI WALINDE VYANZO VYA MAJI

………………….

Waziri
wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewataka wananchi kulinda mazingira ya vyanzo vya
maji kwa kuacha kukata miti ovyo na kufanya shughuli za kibinadamu ili kuepuka
ukame.
 

Ametoa
wito huo mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho wakati wa Maadhimisho ya
Siku ya Mazingira Duniani leo Juni 2, 2025 yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
 

Mhe.
Aweso amesema kuwa uwepo kwa
rasilimali za maji toshevleu ni usalama wa taifa kwakuwa
uwepo wa maji ni uhakika wa chakula, nishati ya umeme pamoja na mipango ya
kimaendeleo ambapo yote hayo yanategemea na mazingira endelevu.

Pia,
Waziri Aweso alisema ni wakati sasa Watanzania watambue kuwa athari za
mazingira ziwe funzo, akitolea mfano Mto Ruvu mkoani Pwani ulivyokauka kutokana
na mabadiliko ya tabianchi ambayo yalisababishwa na binadamu wenyewe.
 

“Athari
za mazingira ziko wazi kwa mfano ukienda Pangani athari zikio wazi, leo tunaona
bahari imekula mji na hivyo kina cha maji kinaongezeka kina kwahiyo changamoto
hizi za kimazingira tunazoziona sasa ziwe funzo kwetu,” alisema.
 

Pamoja
na changamoto hizo, alishukuru na kuipoingeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuandaa
mikakati thabiti na hatua madhubuti inazochukua katika kuyasimamia na kuyatunza
mazingira.

Amesema
hayo yote yanafanyika kutokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni kinara wa kusimamia agenda ya
mazingira.

“Nashukuru
kwa kupata nafasi ya kutembelea mabanda haya, hakika Ofisi ya Makamu wa Rais mmejipanga
na sisi kama Wizara ya Maji tutaendelea kushirikiana na wadau wote katika
kuyalinda na kuyatunza mazingira ili kuhakikisha Tanzania inakuwa bora na salama,
kama mtakumbuka tumefanya mabadiliko ya Sera ili yaendane na mazingira,”
alisema Mhe. Aweso.

 

Maonesho
hayo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanatarajiwa
kuhitimishwa Juni 5, 2025 ambayo ndio kilele.

 

Related Posts