Yanga Yagomea Kikao, Wanataka Hela Ya Ubingwa Tu – Global Publishers


Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira nchini TFF, Cliford Ndimbo.

CLIFORD Ndimbo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) amesema kuwa Yanga SC wamegoma kuongea na kuacha barua licha ya kuitwa na Katibu Mkuu Wilfred Kidao.

Juni 10 2025 TFF walitoa taarifa kuhusu ufafanuzi wa fedha za malipo ya zawadi ya bingwa wa CRDB Federation Cup ambazo Yanga SC walibainisha kuwa hawajapewa na katika barua hiyo TFF walieleza kuwa Yanga SC waliomba kwa maandishi fedha zao za ubingwa zikatwe moja kwa moja kwa malipo ya wachezaji wa kigeni.

Katika taarifa hiyo TFF iliwaambia Yanga SC wafike saa 4 asubuhi wakiwa na nyaraka zote za fedha ili kufanya ukaguzi.

Ndimbo amesema: “Klabu ya Yanga wamefika wameleta barua na kuondoka na wamesema hawana chochote cha kuzungumza, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao alimuita CEO wa Yanga wazungumze alikataa.

“Hizi ni taasisi kubwa na sio kila jambo tunapaswa kuandikiana barua kama tunatoa posa. Kama CEO wa Yanga SC hajui bingwa anapata nini kwanini wanasema wanadai kiasi hicho cha fedha wanachosema.”

Kwa upande wa CEO wa Yanga SC, Andre Mtine ameweka wazi kuwa wao ambacho wanahitaji ni hela ya ubingwa na sio kitu kingine.

“Sisi hatutaki chochote zaidi ya zawadi yetu ya ubingwa kama kuna jambo lolote watuwasilishie kwa njia ya maandishi ila kwasasa hatuhitaji jambo lolote zaidi ya zawadi yetu ya ubingwa.

“Wewe umeshawahi kuona wapi Duniani kote hela ya madeni ikakatwa kwenye hela ya zawadi za ubingwa? Kwanza mnajua thamani ya fedha ya bingwa? Na wapi wametangaza thamani ya fedha za ubingwa?.”

Wasiliana na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.

Related Posts