Bara kama Zanzibar, bima ya watalii ikibisha hodi

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amependekeza kufanyika kwa marekebisho kwenye Sheria ya Bima, Sura 394 ili kuanzisha bima ya usafiri kwa wageni wanaoingia hapa nchini kwa kiwango cha dola za Marekani 44 kama ilivyo kwa upande wa Zanzibar.

Oktoba 1,2024 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia ofisi ya Rais, Fedha na Mipango ilianzisha mpango wa bima za safari kwa wageni wote wanaoingia Zanzibar.

Kufikia Machi 31,2015 kiasi cha Dola za Marekani milioni 20.034 sawa na Sh53.270 bilioni zilikusanywa.

Akiwasilisha bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Waziri Nchemba amesema  bima hiyo  ni kwa ajili ya dharura za kiafya zinazohusiana na safari kwa wageni wanapokuwa hapa nchini, kupotea kwa mizigo ya wageni, kugharamia wageni wanapoondoshwa kwa lazima au ikitokea hatari yenye kulazimu uondoshwaji.

“Bima hii itakuwa na ukomo wa hadi siku 92 kwa mgeni ndani ya muda huo na haitahusisha raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

Amesema  utaratibu huo utakuwa wa ubia kati ya sekta binafsi na Serikali ikiwakilishwa na Shirika la Bima la Taifa, ambapo mgawanyo wa mapato utabainishwa ili kuweka ufanisi katika uendeshaji wake.

Related Posts