……..
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
Kwa mujibu wa Taarifa ambayo imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt Moses Kusiluka imeeleza kuwa Msaju anachukia nafasi ya Profesa Ibrahim Juma ambaye amestaafua.
Aidha imeeleza Uapisho wa Jaji Mkuu utafanyika tar 15 JUNI 2025 Ikulu Chamwino Dodoma.
Ikumbukwe kuwa Jaji Masaju amewahi kuwa na nafasi mbalimbali ikiwemo pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali