PPAA YASHIRIKI KONGAMANO LA MWAKA LA UNUNUZI WA UMMA, KUTOA ELIMU KWA WADAU WA UNUNUZI

:::::::

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imeshiriki Kongamano la Mwaka la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025 kwa lengo la kutoa elimu wa wadau wa ununuzi nchini.

PPAA imetumia Kongamano hilo lililoratibiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Jijini Arusha ili pamoja na mambo mengine iweze kutoa elimu ya moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa (Complaint and Appeal Management Module) katika mfumo wa NeST.

Akiongea kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando wakati wa kuwasilisha mada iliyohusu uzoefu wa kushughulikia malalamiko na rufaa za zabuni kupitia mifumo ya kidijitali, Mkuu wa Sehemu ya Huduma za Sheria za Mamlaka (PPAA), Bi. Agnes Sayi amesema baada ya serikali kuweka sharti la lazima ununuzi wa umma kufanyika kidigitli, Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa imerahisisha zoezi la kuwasilisha malalamiko pamoja na kuokoa muda na gharama.

“Kupitia moduli, wazabuni na Taasisi nunuzi wanaweza kufuatilia mchakato unaoendelea wa rufaa/malalamiko yaliyowasilishwa ambapo mhusika anaweza kupata taarifa zinazohusiana na mchakato wa zabuni,” amesema Bi. Sayi

Kuhusu uzoefu wa kushughulikia malalamiko na rufaa, Bi. Sayi amesema mfumo umesaidia kupunguza masuala ya udanganyifu wakati wa kuwasilisha zabuni kwa kuwa taarifa zinachujwa moja kwa moja na mfumo tofauti na awali ambapo mzabuni anaweza wasilisha taarifa za kampuni tofauti.

Kongamano hilo lililoanza tarehe 13 – 17 Juni, 2025 limehudhuriwa na washiriki takriban 1,000 linaongozwa na kauli mbiu: Ununuzi wa Umma Kidijitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi maalum kwa ukuaji wa uchumi Jumuishi.

 *Mwisho….*

Related Posts