Mfanyakazi wa CRDB afariki akifanya mazoezi Daraja la Tanzanite

Dar es Salaam. Mfanyakazi wa benki ya CRDB, Stanley Josiah amefariki dunia akiwa anafanya mazoezi kwenye Daraja la Tanzanite.

Taarifa za kifo chake hicho zimethibitishwa leo Jumamosi Juni 14,2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano

Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, alipozungumza na Mwananchi Didital.

Tully amesema mpaka mauti yanamkuta, Josiah  alikuwa mkuu wa kitengo cha operesheni za mikopo Benki ya CRDB.

“Benki imepoteza mtu mahiri sana hivyo menejimenti na wafanyakazi inaungana na familia yake katika safari hii ya mwisho,” amesema Mwambapa ambaye ameeleza kuwa msiba upo nyumbani kwa marehemu, Tabata Kinyerezi.

 “Benki inashirikiana na familia tangu taarifa ya ajali ilipotokea hadi sasa kufanya maandalizi yote muhimu hadi siku ya kumpumzisha mwenzetu kwa taratibu tulizojiwekea kama benki,”amesema na kuongeza kuwa, mwili wa marehemu unatarajiwa kupumzishwa Jumanne ijayo Juni 17, 2025 nyumbani kwako huko mkoani Mbeya.

Hata hivyo taarifa ambazo Mwananchi imezipata, zinasema alifika asubuhi mapema ofisini na kuacha gari yake ofisini kwa ajili ya kwenda kufanya mazoezi ya kukimbia.

Chanzo hicho cha habari kinasema , mara nyingi hufanya hivyo kila siku asubuhi.

Related Posts