BALOZI NCHIMBI AFUNGA KONGAMANO LA WAFUGAJI

Matukio mbalimbali katika picha, yakionesha kongamano la wafugaji lililofanyika mkoani Simiyu, Wilaya ya Bariadi, katika viwanja vya Nyakabindi, ambapo mgeni rasmi, aliyelifunga leo Jumapili, tarehe 15 June 2025, alikuwa ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.

Read More

Serikali yaipongeza Green Acres kwa kusomesha wasio na uwezo

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imepongeza mchango wa shule binafsi katika elimu na imezitaka shule hizo kwenda sanjari na mabadiliko ya teknolojia duniani ili kutoa wahitimu wenye uwezo wa kujiajiri na kuajiri wenzao. Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolph Mkenda, kwenye hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Elimu…

Read More

Vikongwe 138 waliuawa 2024, sababu yatajwa

Shinyanga. Vikongwe 138 nchini wameuawa katika kipindi cha mwaka 2024 huku imani za kishirikina zikitajwa kuchochea mauaji hayo. Kufuatia matukio hayo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Khamis amelaani mauaji hayo huku akisema Serikali haitomfumbia macho atakayebainika kuhusika.  Akizungumza leo Juni 15, 2025 kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa…

Read More

DKT. ADESINA AMALIZA ZIARA YA SIKU 4 TANZANIA

::::::: Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Akinwumi Adesina amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 4 aliyoifanya nchini Tanzania kuanzia tarehe 12 hadi 15 Juni 2025. Dkt. Adesina aliondoka nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kusindikizwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje…

Read More

NeST yatajwa kuleta matunda, Serikali yatoa maagizo

Arusha. Matumizi ya mfumo mpya wa kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST), yametajwa kuongeza uwazi, uwajibikaji na kuleta thamani ya fedha katika manunuzi pamoja na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa. Mafanikio mengine yaliyochangiwa na mfumo huo yanatajwa kuwa ni pamoja na uboreshaji wa mazingira na kupungua kwa gharama za kufanya manunuzi kwa wazabuni na Serikali….

Read More

Nchimbi Ashiriki Kongamano la Wafugaji- Apongeza Mabadiliko Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Na Diana Byera, Simiyu. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Emmanuel Nchimbi, ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka minne, ikiwemo kuongezeka kwa mchango wa wizara hiyo katika Pato la Taifa hadi kufikia asilimia 6. Dr. Nchimbi ameshiriki kongamano kubwa la wafugaji lililofanyika katika Uwanja…

Read More