SMZ na mkakati wa kuifungua Pemba kiuwekezaji

Unguja. Katika kufanikisha mipango ya kuifungua Pemba kiuwekezaji, kwa mara ya kwanza linafanyika kongamano kubwa la uwekezaji kisiwani humo

Kongamano hilo linalotarajiwa kufunguliwa kesho Juni 16, 2025 na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, litashirikisha wadau mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki, lengo ni kuzitangaza fursa zinazopatikana katika kisiwa hicho.

Eneo hilo lenye ukubwa wa hekta za mraba 800.8, tayari limeanza kupokea wawekezaji na Serikali imeanza kuboresha miundombinu yake kwa kujenga barabara yenye urefu wa 15, imejengwa na umeme umeanza na maji na intaneti vimeanza kuwekwa.

Akizungumza leo Juni 15, 2025, baada ya kufanya matembezi ya hisani litakapofanyika kongamano hilo katika eneo huru la uwekezaji Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Katibu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Zena Said amesema ni wakati wa Pemba, sasa kufunguka kwa uwekezaji.

Ametumia fursa hiyo kuwataka wazawa kutumia fursa hiyo pia kuwekeza badala ya kudhani uwekezaji unaotakiwa ni kwa wageni pekee.

“Huu ni wakati wa Pemba, Serikali imeamua kwa makusudi kuifungua Pemba na ndio maana imeleta kongamano hili katika kuonyesha fursa mbalimbali zilizopo kama inavyofanyika Unguja.

“Tuna lengo la kuifungua Pemba kupitia Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar (Zipa) na hili kongamano ni sehemu ya mikakati hiyo,” amesema.

Amesema Serikali inaweka mazingira bora kwa uwekezaji na kutoa elimu kwa wananchi namna wanavyoweza kunufaika na uwekezaji huo kwa kushiriki fursa mbalimbali.

Naye Mkurugenzi wa Zipa, Saleh Saad Mohamed amesema wamejipanga kuifungua Pemba ikiwa ni sehemu ya visiwa vya Zanzibar katika uwekezaji na ndio maana Serikali imeamua makusudi kufanya kongamano hilo katika kisiwa hicho eneo la Micheweni.

Eneo hili lina ukubwa wa hekta 800.8 ambalo tayari limeanza kupokea wawekezaji na Serikali imeanza kuboresha miundombinu yake kwa kujenga barabara yenye urefu wa kilometa 15, imejengwa miundombinu ya umeme na maji na intaneti vimeanza kuwekwa.

Hatua hiyo, kwa mujibu wa Saleh, inalenga kuwavutia wawekezaji ili wakifika wasipate changamoto yoyote.

Amesema imefanya mabadiliko ya sheria namba 14 ya uwekezaji ya mwaka 2018 na sasa kuna sheria namba 10 ya mwaka 2013. Amesema pia itatarajiwa kusainiwa mwongozo wa uwekezaji wa mwaka 2024.

Eneo hilo linapangwa kuwekeza zaidi sekta za nyumba za makazi, hoteli, huduma za hospitali na shule, Tehama.

Kwa kuzingatia umuhimu wa Vijana na ubunifu wao Serikali imetenga eneo maalumu kwa biashara changa (startups).

Related Posts