Samia Afungua Kiwanda Kitakachoinufaisha Wakulima wa Pamba – Video – Global Publishers



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Juni 16, 2025, amefungua rasmi kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji wa pamba cha MOLI Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi, Mkoa wa Simiyu.

Kiwanda hicho kinatarajiwa kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wa pamba na kuboresha upatikanaji wa vifaa vya ujenzi wa miundombinu ya maji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na maeneo mengine ya nchi.

Rais Samia akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha MOLI Oil Mills Co. Ltd Milembe Gugu Silanga kuhusu utengenezaji wa mabomba ya maji na uchakataji wa pamba kabla ya ufunguzi wa kiwanda hicho Bariadi mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.

 

 











Related Posts