VIDEO: Lissu aomba ajitetee mwenyewe mahakamani, ataja sababu

Dar es Salaam. Mwenyekiti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ameomba mahakamani ajitetee mwenyewe huku akitaja sababu ni kuwa mawakili wake kutopewa nafasi ya faragha kuzungumza naye gerezani.

Lissu amebainisha hayo leo Jumatatu Juni 16, 2025 wakati kesi yake ikianza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Lissu anakabiliwa na kesi ya uhaini pamoja na kesi kesi ya kuchapisha taarifa za uwongo mtandaoni.

Kesi hizo ambazo zinasikilizwa na mahakimu wawili tofauti zote zinaendelea leo lakini katika hatua tofautitofauti.

Wakati kesi ya uhaini leo inatajwa kwa ajili ya Serikali kutoa mrejesho wa hatima ya upelelezi ulikofikia, kesi ya kuchapisha taarifa za uwongo imepangwa kwa ajili ya kuanza usikilizwaji rasmi, yaani Mahakama kuanza kupokea ushahidi wa upande wa mashtaka.



Lissu aibua mazito mahakani, asimulia magumu

Hata hivyo kuanza kwa usikilizwaji wa kesi hiyo leo kunategemea na mrejesho wa hatima ya shauri dogo la maombi lililofunguliwa na Jamhuri kuhusiana na ulinzi wa mashahidi wake wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi

Related Posts