TET YAKUSANYA BILIONI 2, DKT KOMBA AKIHIMIZA WADAU KUNUNUA VITABU ZAIDI

…………..

Taasisi ya Elimu nchini (TET), imekukusanya fedha taslimu zaidi ya Sh 2 bilioni ikiwa ni sehemu ya mkakati wa ukusanyaji wa Sh35 bilioni wenye lengo la kufanikisha lengo la “Kitabu Kimoja cha Somo Moja kwa Mwanafunzi Mmoja’.

Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba wakati wa kilele cha Jubilii ya miaka 50 ya taasisi hiyo yaliyofanyika makao makuu ya TET, Dar es Salaam.

“Hadi kufikia Juni 16, 2026 TET imekukusanya fedha taslimu zaidi ya Sh 2.6 bilioni huku ahadi zilizopokelewa kutoka kwa wadau zinafikia zaidi ya Sh4 bilioni.” ameongeza Dkt. Komba

Katika hafla hiyo wachangiaji waliotoa michango ya zaidi ya Sh25 milioni walipewa vyeti maalum vya shukrani vilivyokabidhiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Miongoni mwa wachangiaji hao ni wachapishaji maarufu wa maudhui ya elimu Nyambari Nyangwine Group of Companies waliochangia Sh110 milioni.

Dkt. Komba ameendelea kuwasihi wadau wa elimu kuchangia mpango huo ili kuwezesha lengo la kila mwanafunzi kwa ngazi za elimu ya msingi na sekondari.

 

Related Posts