Dereva wa boti ya uokoaji Ziwa Victoria asimulia magumu anayopitia barabarani

Dereva wa gari linalosafirisha boti maalumu ya uokoaji katika Ziwa Victoria (Ambulance Mwanza), Hamidu Mshamu ameeleza changamoto anazokumbana nazo akiwa katika safari ya siku 14 kutoka Mtwara hadi Mwanza.

Akizungumza na Mwananchi Digital akiwa mkoani Morogoro leo Alhamisi Juni 19, 2025, Mshamu amesema tayari ametembea zaidi ya kilomita 1,100 tangu kuanza safari hiyo na kwa siku huweza kusafiri kati ya kilomita 100 hadi 110 kutokana na hali ya miundombinu na mazingira ya barabara. “Maeneo mengine tunalazimika kusimama kukata miti ili isiathiri mzigo wetu mkubwa,” amesema.

Boti hiyo baada ya kuwasili eneo la Msamvu, Morogoro, imepokewa na mamia ya wananchi.   


Ofisa Mahusiano wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (Tasac), Mariamu Mwayera amesema boti hiyo imenunuliwa kupitia mradi wa kikanda wa usafirishaji na mawasiliano Ziwa Victoria.
Zaidi mtazame kwenye picha mjongeo yetu hapo juu.

Related Posts