Shamrashamra zimeendelea kushuhudiwa katika eneo la Kigongo-Busisi lilipo Daraja la JP Magufuli, linalotarajiwa kuzinduliwa leo, Alhamisi Juni 19, 2025.
Vijana waliovalia sare za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wengine wakiwa na fulana zenye maneno yanayoeleza utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan, wamefurika maeneo hayo ikiwa ni shamrashamra kuelekea uzinduzi huo.
Nderemo na vifijo hivyo, vinafanyika wakimsubiri Rais Samia Suluhu Hassan kufika mkoani Mwanza kwa ajili ya uzinduzi rasmi.
Endelea kufuatilia mitandao ya Mwananchi