Dar City wanatupia tu BDL

Dar City inaongoza  kwa kufunga pointi 756, katika Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam (BDL).

Dar City imefunga pointi hizo, kutokana na michezo nane, ikiongoza pia katika msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 16.

Inayofuatia ni Savio  iliyofunga pointi 654, Stein Warriors 594, JKT 580, KIUT  538, Srelio 523, Kurasini Heat 497, ABC  493 na Vijana ‘City Bulls’ 492.

Nyingine ni Mchenga Stars 485. Pazi 467, UDSM 440, Chui 418, Polisi, 402, na Mgulani JKT 387 .

Kocha wa kikapu wa Dar City, Mohamed Mbwana alisema ligi ya  mwaka huu imekuwa na ushindani mkubwa tofauti na miaka ya nyuma.

“Ushindani huu ndiyo unaotakiwa, nachojua kupitia mashindano haya  viwango vinaweza vikaongezeka,” alisema Mbwana.

Related Posts