Jeshi la Polisi Lafafanua Ukamatwaji wa Wachokonozi – Video – Global Publishers



Jeshi la Polisi limesema linawashikilia Vijana wawili wanaojulikana kwa jina la Wachokonozi ambao ni Joseph Mrindoko (37) na Jackson Kabalo (32) kwa tuhuma za matumizi mabaya ya Mtandao, ambao awali taarifa zilizosambaa Mtandaoni zilidaiwa wamechukuliwa na Watu Wasiojulikana waliokuwa na silaha

Taarifa ya Polisi ya Juni 21, 2025 imesema Watuhumiwa hao walikamatwa na Jeshi la Polisi mnamo Juni 20, 2025

Aidha, katika taarifa hiyo Jeshi la Polisi limeonya watumiaji wa Mitandao ya Kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika nazo zinazoleta taharuki katika Jamii, hasa zile za kuzusha kuwa Watuhumiwa wamekamatwa na Watu Wasiojulikana jambo ambalo sio la kweli.











Related Posts