Pangua ya Rais Samia yawaacha wakuu wa mikoa watano

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na kuwahamisha watendaji wake, ambapo amewaweka kando wakuu wa mikoa (RC) watano akiwemo Paul Makonda wa Arusha.

Mbali na Makonda aliyeachwa, wengine na mikoa yao kwenye mabano ni, Peter Serukamba (Iringa), Thomas Andengenye (Kigoma), Dk Juma Homera (Mbeya) na Daniel Chongolo wa Songwe.

Mkeka huo umetolewa usiku wa leo Jumatatu, Juni 23, 2025 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ikimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kisiluka.

Uteuzi huo umefanyika siku nne zimesalia kabla ya dirisha la uchukuaji na urejeshaji fomu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufunguliwa saa 2 asubuhi ya Juni 28, 2025.

Duru za siasa zinawataja baadhi ya wakuu hao wa mikoa kwenda kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali nchini.









Mathalani, Makonda anatajwva kujitosa Arusha Mjini, Serukamba  inaelezwa anakwenda Kigoma Kaskazini, Dk Homera anakwenda Namtumbo huku Chongolo ikielezwa anajitosa Makambako.

Related Posts