………..
Na Ester Maile Dodoma
Bangi imeendelea kuwa dawa ya kulevya iliyokamatwa nchini kwa kiwango kikubwa kwa mwaka 2024 ikiwa ni jumla ya tani 2,302.37.
Hayo yameelezwa mbele ya waandishi wa Habari jijini Dodoma na William Lukuvi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu)
“leo June 23,2025 amesema kuwa”kati ya hizo, tani 2,303.2 ni bangi iliyozalishwa nchini na tani 4.17 ni bangi yenye kiwango cha juu cha kemikali ya THC maarufu kama Skanka, iliyoingizwa nchini kutoka katika baadhi ya nchi za Kusini mwa Afrika. “ Waziri Lukuvi
Katika hatua nyingine Lukuvi amesema kuwa kiasi cha Skanka kilichokamatwa kimeongezeka kwa asilimia 89.8 ikilinganishwa na mwaka uliopita, ikiwa ni ishara ya kuimarika kwa udhibiti wa biashara ya dawa hizo nchini.
Katika hatua nyingine ameongeza kuwa madawa ya kulevya aina ya mirungi imekamatwa kwa kiasi kikubwa ambapo jumla ya tani 18.45 zilikamatwa katika operesheni mbalimbali kote nchini.
Pia amesema kuwa kwa upande wa dawa za kulevya zinazozalishwa viwandani, Serikali ilifanikiwa kukamata tani 1.7 za methamphetamine, kilogramu 433.02 za heroin na gramu 853 za cocaine.
Pamoja na hayo amempongeza Rais Samia kwa dhamira yake ya mapambano dhidi ya biashara haramu ya madawa ya kulevya kwa kuiwezesha Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya na vyombo vya ulinzi na usalama wataalamu wa afya ,wadau katika mapambano na wananchi wote kwa kushirikiano mkumbwa uliosaidia kufikia mafanikio