Askari wa Jeshi la Magereza Kizimbani kwa Kosa la Kumlawiti – Video – Global Publishers



Askari wa Jeshi la Magereza amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, akikabiliwa na kesi ya kumlawiti mtoto wa miaka 13.

Askari huyo alifikishwa mahakamani jana, Juni 24, 2025, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Ruth Mkisi, na kusomewa shtaka moja la ulawiti.

Awali, Juni 14, 2025, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Abel Mtagwa, alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kueleza kuwa taratibu za kijeshi dhidi ya askari huyo zinaendelea, na baada ya kukamilika, hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.











Related Posts