…………….
Kamati
ya Ushauri ya Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Kitaasisi wa
Utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (EMA) imekutana kwa ajili ya
kujadili na kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 jijini Dodoma leo Juni 25,
2027.
Kikao
hicho kimeongozwa na Bw. Wanjara Jandwa kutoka Kitengo cha Huduma za
Sheria cha Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambaye
aliwapongeza kwa kazi nzuri ya kutoa maoni yenye kujenga.
Bajeti
hiyo iliyowasilishwa na Mratibu wa Mradi Bw. Richard Masesa imejadiliwa na
wajumbe walioshiriki kikao hicho kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, NEMC, Wizara
za kisekta na halmashauri.
Mradi wa EMA unaosimamiwa na Ofisi
ya Makamu wa Rais, unafadhiliwa
na Serikali ya Sweden kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sweden (SIDA),
unakusudia kushughulikia changamoto kuu za mazingira na kuondoa vizuizi vya
kisekta vilivyopo katika Wizara na mamlaka maalumu za kisheria na kuongeza
wigo wa utendaji.
Kwa
mantiki hiyo, mradi huo ni nyenzo mojawapo ya kuboresha uratibu wa
usimamizi wa mazingira nchini unaokusudia kushughulikia changamoto kuu za
mazingira.