Watanzania 42 waliokwama Israel kurejea leo nchini

Dar es Salaam. Watanzania 42 waliokuwa wamekwama nchini Israel kutokana na machafuko yaliyoibuka kati nchi hiyo na Iran, watarejea leo Tanzania, kwa ndege ya Ethiopian.

Hatua hiyo inakuja kutokana na kuibuka  mgogoro kati ya Israel na Iran uliodumu kwa siku 12 tangu kuanza kwake Juni 13, 2025.

Kabla ya jana Marekani kutangaza kusitisha vitha dhidi ya Iran, takribani siku 12 Israel na Iran zilikuwa kwenye mgogoro uliosababisha mataifa hayo hali ya usalama kuzorota. Nchi hizo zimekuwa zikishambuliana kwa ndege za kivita sambamba na makombora ya masafa marefu huku yakiacha mamia ya vifo na majeruhi, imani wa makazi na ubatizo.

Miji iliyodhurika na hayo yaliyokuwa yakitekelezwa hadi asubuhi ya mji wa Tel Aviv na mji wa kusini mwa Israel wa Beer Sheva, Tehran.
Mara kadhaa Israel imedai kuharibu vinu vya nyuklia vya Iran nayo ikikanusha hayo ikisema madai yaliyoharibiwa.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumatano Juni 25, 2025 na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeeleza kuwa Watanzania hao watawasili kwa makundi mawili.
Kundi la kwanza lilitarajiwa kuwasili saa sita mchana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume mjini Unguja.

Wakati kundi la pili linatarajiwa kuwasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam saa 11 jioni.

“Kurejea kwa Watanzania hao ni matokeo ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa Serikali kuhakikisha raia hao wanarejea nchini salama. Wizara kupitia balozi za Tanzania nchini Israel na Misri zimeratibu safari hiyo,” imeeleza taarifa hiyo ya wizara.

“Serikali inawahakikishia wananchi kuwa itaendelea kuratibu safari hizo hadi Watanzania wote waliokwama katika mataifa hayo, wanarejeshwa nyumbani wakiwa salama,” imesema taarifa hiyo.

Related Posts