
Wajumbe CCM wageuka lulu majimboni
Dar es Salaam. Kama ambavyo ungetamani shuka nyakati za baridi na chandarua panapo mbu, ndivyo walivyo muhimu wajumbe katika kipindi hiki ambacho Chama cha Mapinduzi (CCM), kinafungua pazia la mchakato wa ndani wa kuwapitisha wagombea wa udiwani, ubunge na uwakilishi. Umuhimu wa wajumbe, unatokana na jukumu lao katika mchakato huo –kupiga kura za maoni zinazoamua…