Maisha yaanza kurejea Tehran, Tel Aviv baada ya mapigano makali

Tehran. Baada ya siku 12 za piga nikupige kati ya Iran na Israel kufuatia mzozo wa kile kilichodaiwa vinu vya nyuklia vya Iran sasa imeelezwa shughuliz imeanza kurejea kama illivyokawaida katika jiji la Tehran na Tel Aviv maeneo yaliyokuwa kama shabaha kwa sehemu kubwa. 

Katika mapigano makali ya mabomu yalivyodumu karibu wiki mbili mamia ya watu waneuawa wenginr wakijeruhiwa huku makazi yakiharibiwa vibaya hali iliyosababisha wakaazi kukimbia.

Baada ya mapigano hayo Marekani pia ilitangaza kusitisha vita dhidi ya Iran baada ya kudaiwa kuingilia kati kwa kushambulia vinu vya nyukilia hali iliyosababisha mataifa hayo usalama kuzorota.

Awali, kulikuwa na sintofahamu ambapo Marekani inadai kuviharibu kabisa vinu vya nyukilia vya Iran huku yenyewe ikisema kila kitu kiliratibiwa mapema na kwamba uharibifu haukuwa mkubwa kama Marekani inavyodai.

Hata hivyo, mshauri wa mambo ya nje wa ikulu ya Urusi Yuri Ushakov amesema nchi yake imekaribisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya pande hizo mbili hasimu na inatumai yatadumu. 

Kufuatia mapambano hayo makali kusitishwa hali nchini Iran hasa katika jiij la Tehran imeanza kurejea kama ilivyokuwa awali.

Ingawa biashara zimeanza tena na wakazi wamerejea mitaani wakienda sokoni wengine wakikatiza mitaani jambo ambalo wakati wa vita haikuwa hivyo kwa mujibu wa France 24 baadhi ya wakazi wanawasiwasi wa kwamba usitishaji vita hivyo unaweza usidumu.

Katika soko la Tajrish kaskazini mwa Tehran, baadhi ya wakazi wametoa maoni yao juu ya usitishaji vita wakisema huenda zuio lisidumu ingawa wao wanataka amani.

“Sidhani kama inaweza kudumu, Tungependa usitishaji vita… lakini inawezekana wasitekeleze ahadi zao,” amesema Ahmad Barqi, mfanyabiashara wa vifaa vya elektroniki mwenye umri wa miaka 75.

Hata hivyo, hakuna mashambulizi yaliyorekodiwa Tehran tangu asubuhi na mapema kuanzia jana Jumatano, baada ya usiku ambao wakazi waliamshwa na milipuko mingi zaidi kuliko hapo awali.

Imeelezwa mashambulizi ya usiku kucha ya Israel yaliwafanya wakazi wa Tehran kuwa na wasiwasi wa kuendelea kwa vita.

Mgogoro huo umeathiri maisha ya kiuchumi Tehran, huku idadi kubwa ya biashara pamoja na ofisi za umma zikilazimika kufunga wakati ofisi binafsi katika vitongoji vilivyo hatarini zaidi zikiwa zimetatelekezwa.

Mashambulizi ya Israel yaliharibu majengo ya umma, hasa yale yanayohusiana na jeshi, Walinzi wa Mapinduzi au mpango wa nyuklia wa Iran, pamoja na kuua raia katika majengo ambapo maofisa wa ngazi za juu na wanasayansi waliishi.

Idadi kubwa ya watu wamerudi Tehran, kuendeleza na kazi kwaajili ya kupata kipato kuendeleza na maisha.

Katika miji ya Tel Aviv na Haifa napo Waisraeli wamepokea kwa furaha hali ya maisha kurejea kawaida.

Kwa mujibu wa Reuters jana jumatano shule zimefunguliwa huku watoto wakienda kwa mara ya kwanza tangu mapambano makali ya siku 12.

Kwa upande wa Israel wakati wa mapambano na Iran, familia nyingi zenye vyumba salama ndani ya nyumba zao zilitumia muda mwingi huko, huku wale waliotegemea makazi ya umma walikimbia huko kila mara kulipotokea tahadhari,

Israel ilianza kuishambulia Iran Juni 13, ikisema inalenga kuharibu uwezo wa nyuklia wa adui wake huyo.

Katika mji wa kaskazini wa bandari wa Haifa, watu wameonekana wakinywa kahawa na juisi za matunda kwenye migahawa, wakisoma magazeti.

Related Posts