Hapo jana tumeshuhudia hitimisho la ligi kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2024/25 kwa mchezo wa derby ya Kariakoo kati ya mwenyeji Yanga dhidi ya Simba ambapo mchezo ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na hivyo kutawazwa rasmi kuwa mabingwa wa NBC Premier league kwa 2024/25. Ushindi huu haukua kwa mashabiki wa timu pekee bali ulikua kwa wabashiri wa meridianbet waliosuka majamvi yao kwa machaguzi mengi na yenye odds kubwa yaliyokuwepo.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Pacome Zouzua kwa mkwaju wa penalty pamoja na Clement Mzize dakika za jioni kabisa na Yanga kuweka historia ya kulibeba kombe hilo kwa mara ya 31 huku timu hiyo ikijikusanyia alama 82 na mtani wao Simba akibaki nafasi ya pili kwa jumla ya alama 78.
Msimu huu ulikua na jumla ya timu 16 na kila timu ilicheza jumla ya michezo 30 (15 nyumbani na 15 ugenini). Timu za Yanga, Simba, Azam na Singida Black Stars zimefanikiwa kumaliza kwenye nafasi nne za juu hivyo kujikatia tiketi ya moja kwa moja kushiriki michuano ya kimataifa ambapo Yanga na Simba watashiriki michuano ya klabu bingwa msimu ujao huku Azam na Singida wakishiriki michuano ya kombe la shirikisho.
NB: Jiunge na Meridianbet na ujionee ushindi rahisi kupitia michezo mbalimbali ya kasino ya mtandaoni. Pia unaweza kuongeza kipato chako kwa kubashiri mechi zenye ODDS KUBWA. Piga *149*10# au tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz
Kuisha kwa msimu huu kumekua na huzuni kwa baadhi ya timu ambazo zimeshuka daraja huku wengine wakisubiri kucheza michezo ya mtoano ili kujua hatima yao. Klabu za Kagera sugar na Ken Gold zimeshuka moja kwa moja ili kuzipa nafasi Mtibwa Sugar na Mbeya City zilizopanda daraja huku Tanzania Prisons na Fountain Gate wakisubiri mechi za mtoano dhidi ya Stand United na Stand United.
Takwimu za wachezaji kwa msimu huu zimekua na mchuano mkubwa kuanzia kwa Kinara wa mabao ambapo Ahoua wa Simba ameongoza kwa kuwa na jumla ya mabao 16 akifuatiwa na Mzize mwenye magoli 14.
Msimu huu tumeshuhudia hat trick ya kwanza ya msimu kutoka kwa Prince Dube dhidi ya mashujaa lakini pia Jean Ahoua kwenye mchezo dhidi ya Pamba jiji, Steven Mukwala dhidi ya Coastal Union, pamoja na ile ya Stéphane Aziz Ki dhidi ya KMC. Huku mchezaji aliyeshika vichwa vya wengi akiwa ni Sowah wa Singida BS aliyesajiliwa dirisha dogo na kufanikiwa kufunga mabao 12 kwenye michezo 12 aliyocheza.
Upande wa walinda mlango, golikipa wa Simba, Mousa Camara ameibuka kinara wa Clean sheet kwa kucheza jumla ya michezo 19 bila kuruhusu bao na kuifikia rekodi iliyowekwa na Aishi Manura msimu wa 2017/18 lakini alishindwa kuivunja rekodi hiyo kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Yanga kwa kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara mbili.
Moja ya kumbukumbu za msimu huu ni pamoja na kushuhudia mchezo wa mwisho ukiruhusu matumizi ya waamuzi wa kigeni jambo ambalo halikuzoeleka hapo kabla lakini pia kugomea michezo kwa timu za Simba na Yanga, hali iliyopelekea kung’olewa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi za juu kwenye bodi ya ligi.
Timu zimeshuhudia safu bora za ushambulizi huku Yanga wakiwa kinara kwa kufunga jumla ya mabao 83 wakifuatiwa na watani wao Simba waliofunga jumla ya mabao 69 huku Pamba Jiji, Kagera sugar na Ken gold wakiwa na safu dhaifu ya ushambuliaji na wote wana jumla ya mabao 22 kwa kila timu.
Na kwa upande wa safu ya ulinzi, Yanga pia wamekua na safu bora ya ulinzi wakiruhusu jumla ya mabao 10 pekee kwenye michezo yote 30 huku Simba wakishika nafasi ya pili kwa kuruhusu mabao 13 pekee kisha Azam walioruhusu 19. Na timu za Ken Gold na Fountain Gate zikiwa na safu dhaifu Zaidi za ulinzi kwa kuruhusu jumla ya mabao 62 kwa 58.
Kumalizika kwa ligi ya NBC kumeacha mabingwa wengi kupitia meridianbet. Jisajili sasa na meridianbet uwe mmoja wa washindi kwa kusuka jamvi lenye faida kubwa kwani huko michezo haiishi.