Arajiga apewa tena fainali FA Yanga vs Singida BS

SHIRIKISHO la Soka Tanzania, limemteua Ahmed Arajiga, kuwa mwamuzi wa kati wa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) utakaozikutanisha Yanga dhidi ya Singida Black Stars.

Arajiga ni mara ya pili mfululizo kuwa mwamuzi wa kati kwenye fainali ya michuano hii baada ya kuteuliwa msimu uliopita Yanga ilipoifunga Azam kwa penalti 6-5.

Mbali na hilo, pia Arajiga alichezesha nusu fainali ya Kombe la FA msimu huu, Singida Black Stars ikiichapa Simba mabao 3-1, huku akitangazwa kuwa mwamuzi wa kati katika Dabi ya Kariakoo, Yanga dhidi ya Simba iliyotarajiwa kuchezwa Machi 8, 2025 kabla ya kuahirishwa Juni 15, 2025 na kuchezwa Juni 25, 2025 waamuzi wakitokea Misri.

Katika fainali itakayochezwa kesho Jumapili Juni 29, 2025 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 2:15 usiku, Arajiga atasaidiwa na Frank Komba ambaye pia alikuwa msaidizi wa Arajiga fainali ya msimu uliopita. Hamdani Said pia atakuwa msaidizi namba mbili. Mwamuzi wa akiba ni Tatu Malogo.

Related Posts