Dar es Salaam. Aliyekuwa mbunge wa viti maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Ester Bulaya ameweka wazi kuwa amerudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitangaza kugombea Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara.
Bulaya aliwahi kuwa mbunge wa viti maalumu (CCM) mwaka 2010 hadi 2015 kabla ya mwaka 2015 kuhamia Chadema ambapo aliwania ubunge wa Bunda Mjini na kumshinda mwanasiasa mkongwe Stephen Wasira.
Novemba 2020 akiwa na wenzake 18 akiwemo Halima Mdee waliingia katika mgogoro na Chadema baada ya kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalumu pasipo kuruhusiwa na chama hicho kikuu cha upinzani.
Tayari baadhi ya wabunge wenzake wametangaza kwenda vyama mbalimbali ikiwemo CCM ili kuwania ubunge wa majimbo na viti maalumu.
Lakini, kwa Bulaya imekuwa tofauti akuweka wazi kama amerejea CCM ila leo Jumamosi Juni 28,2025 ameliambia Mwananchi kuwa amerudi ‘nyumbani’ na ameshakabidhiwa kadi.
” Mimi ni mtu mzima nimesharudi nyumbani na nimeshakabidhiwa kadi yangu kimyakimya bila matangazo. Nitachukua fomu wakati kuanzia leo ili kuwania ubunge wa Bunda Mjini,” amesema Bulaya.