Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemteua Jaji Mkuu mstaafu, Profesa Ibrahim Juma kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Profesa Juma anachukua nafasi ya Dk Stergomena Tax ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Uteuzi huo unakuja ikiwa ni siku 16 tangu Profesa Juma kustaafu wadhifa wa Jaji Mkuu wa Tanzania ambapo Rais Samia alimteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, George Masaju kushika wadhifa huo, ambapo aliapishwa Juni 15, 2025.
Aidha, katika uteuzi huu wa leo Juni 29, 2025 kama taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk Moses Kusiluka ilivyoeleza, Rais pia amemteua Dk Deo Mwapinga kuwa Balozi.
Dk Mwapinga ni Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wabunge wa Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR).