TANESCO YAOMBA RADHI KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA UMEME KUTOKANA NA HITILAFU GRIDI YA TAIFA

::::::::

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa taarifa kwa umma kuwa mnamo majira ya saa 02:36 asubuhi, kumetokea hitilafu kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa ambayo imesababisha kukosekana kwa huduma ya umeme katika mikoa yote inayounganishwa na Gridi hiyo.

 Shirika hilo limesema kuwa Timu ya wataalamu inafuatilia kwa karibu ili kubaini chanzo halisi cha hitilafu hiyo na kuhakikisha huduma ya umeme inarejea haraka. 

TANESCO imeomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na inawaomba wananchi waendelee kuwa watulivu wakati juhudi za kurejesha huduma zikiendelea.


 

Related Posts