BIASHARA YA KABONI NYENZO MUHIMU KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mha. Hamad Yussuf Masauni akizungumza
na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Juni 30, 2025 mara baada ya kupokea
Taarifa ya
Tathmini ya Mwenendo wa Biashara ya Kaboni kutoka kwa Kamati ya Biashara ya
kaboni.

…………………..

Mwandishi Wetu Dar es Salaam

Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mha. Hamad Yussuf Masauni amesema
Biashara ya Kaboni ni miongoni
mwa nyenzo muhimu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambapo nchi,
taasisi, kampuni na wananchi wanaweza kushiriki katika jitihada za Kitaifa na
Kimataifa za kupunguza gesijoto duniani. 

Waziri Masauni amesema hayo jijini Dar es Salaam Juni 30, 2025 mara baada
ya kupokea T
aarifa ya Tathmini ya Mwenendo wa Biashara ya
Kaboni kutoka kwa Kamati ambapo amesema
Tanzania imeimarisha usimamizi wake kwa kuanzisha Kanuni za mwaka 2022 na
marekebisho yake ya mwaka 2023, pamoja na Kituo cha Taifa cha Kuratibu Kaboni
(NCMC).

Amesema NCMC ina jukumu la
kusajili miradi, kuwezesha ufuatiliaji, uthibitishaji wa gesijoto, utoaji wa
elimu na uhamasishaji wa wadau.
Tangu
kuanza kutumika kwa kanuni, jumla ya miradi 73 ambayo miradi 69 ipo katika
hatua mbalimbali za usajili na miradi 4 ipo katika hatua ya utekelezaji.

Ameongeza kwa upande wa Zanzibar imeanza kupokea
maombi ya miradi ya kaboni kufuatia kupitishwa kwa Kanuni za Udhibiti na
Usimamizi wa Biashara ya Kaboni za mwaka 2025. Kufikia Mei 2025, kampuni nne
(4) zilionesha nia ya kutekeleza miradi hiyo, ambapo mbili (2) kati yao
zimewasilisha maandiko dhana
.

“Kamati hii ilipewa jukumu la kufanya tathmini na
kutoa mapendekezo ya kuongeza ufanisi wa uendeshaji wa biashara ya Kaboni nchini,
l
engo kuu ni kufanya tathmini ya hali ya sasa ya biashara ya kaboni nchini
Tanzania na kutoa mapendekezo kwa serikali kuhusu njia bora za kuimarisha
mifumo na mwenendo wa biashara ya kaboni Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema katika kuimarisha
uelewa na ushirikishwaji wa wadau katika Biashara ya Kaboni,
Serikali kwa kushirikiana na
wadau imeendelea kutoa elimu kwa Umma ili kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu
biiashara hiyo.

Amesema Kamati imependekezwa kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Biashara
ya Kaboni, kuandaa miongozo ya mafunzo kwa
wadau wa ngazi zote, pamoja na kuanzishwa
majukwaa ya wadau la majadiliano katika ngazi mbalimbali
.

Utekelezaji
wa Biashara ya Kaboni nchini utaimarika kwa kufanya mapitio ya kanuni na
miongozo ya biashara ya Kaboni, kuboresha rejesta ya Taifa ya Kaboni, kuweka
mkakati mahususi wa utoaji wa elimu kwa umma, kuboresha mifumo ya usimamizi na
utunzaji wa takwimu na kuhamasisha ushirikishwaji wa wadau ikiwemo sekta
binafsi.

Ameongeza kwa upande wa Miradi ya kimkakati kunufaika na Biashara ya
Kaboni,
Tathmini inaonesha kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kunufaika na
Biashara ya Kaboni kupitia utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika sekta
mbalimbali, ikiwemo reli ya kisasa ya umeme (SGR), Mabasi yaendayo haraka (Dar
es Salaam Rapid Transit – DART), uzalishaji wa umeme, gesi asilia, misitu,
kilimo, majengo, elimu, madini, udhibiti wa taka na uchumi wa buluu.
 

Related Posts