:::::::
Aliekuwa mbunge wa Viti maalum kupitia chama cha Democrasia na Maendeleo Chedema Esta Bulaya amechukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la Bunda Mjini kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Ccm
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hiyo Bulaya amesema ameamua kurejea katika chama cha mapinduzi kutokana na chama hicho kumlea kwa miaka mingi katika masuala ya kisiasa.
Bulaya pia amesema kuwa kwasasa amekuwa na furaha kubwa baada ya kurudi chama cha mapinduzi ambapo amesema amechukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Bunda mjini jimbo ambalo kwa miaka ya nyuma alikuwa mbunge
Esta Bulaya kabla ya kuhamia chama cha Democrasia na Maendeleo chadema amewahi kuwa mbunge wa viti maalumu kundi la vijana 2010- 2015 na baadae kutimkia chadema na kugombea ubunge wa jimbo la Bunda 2015 -2020 na kufanikiwa kushinda nafasi hiyo kwa kumshinda Stiven Wasira