::::::::’
KATIKA Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba,kampuni ya Laziz Bakery imeibua mshangao na kuvutia maelfu ya watembeeleaji way maonesho hayo baada ya kutengeneza keki kubwa yenye uzito wa tani 3 sawa na kilo elfu 3, ikiwa ni keki kubwa zaidi kuwahi kutengenezwa Afrika Mashariki.
Keki hiyo si tu ya kipekee kwa ukubwa wake bali pia kwa ujumbe wake imebeba taswira ya uzalendo na kuakisi miradi mikubwa ya uwekezaji inayotekelezwa na Serikali ya Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile miundombinu ya Barabara , afya, elimu na viwanda.
Akizungumza Katika Maonesho hayo yanayofanyika Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya LAZIZ BAKERY limited, Hamza Muzammil ameeleza kwamba ubunifu huo umelenga kuonyesha maendeleo yanayopatikana chini ya mazingira bora ya biashara na uwekezaji yaliyowekwa na serikali ya awamu ya sita.
Kwa upande wake Balozi wa bidhaa za vyakula zinazotengenezwa la Kampuni hiyo ikiwemo keki, Mwijaku amebainisha kwamba ubunifu wa kuweka Miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa na serikali nchini Katika keki hiyo kubwa ni ishara ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kukuza uchumi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Aidha, ameeleza kuwa hatua hiyo ni mfano bora wa namna sekta binafsi inaweza kushirikiana na serikali katika kuhamasisha maendeleo na uwekezaji ndani nchi.