KATIKA kuendelea dhamira yao ya kurejesha kwa jamii wakali wa ubashiri Meridianbet leo hii waliamua kuwafikia wakazi wa Magomeni na Manzese na kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu ikiwemo vyakula ambavyo vitawasaidia kuendesha maisha yao.
Kama tunavyojua jamii yetu ambayo inatuzunguka baadhi yao uchumi wao ni wa kati wengine wa juu na wengine wana uchumi mdogo hivyo wanahitaji kushikwa mkono ili waweze kuishi kama wengine. Uhitaji ni mkubwa katika sehemu nyingi za jiji la Dar es salaam kutoka ana wingi wa watu.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Meridianbet, Nancy Ingram alisema, “Meridianbet tunaamini katika kurudisha kwa jamii. Tunatambua kuna watu wengi wanaopitia magumu na jukumu letu kama kampuni si tu kufanya biashara bali pia kuwa sehemu ya suluhisho. Tumekuwa tukifanya shughuli kama hizi mara kwa mara ili kusaidia jamii zinazotuzunguka.”
Ukija huku kwenye CSR ndio usiseme kila mwezi huhakikisha kufanya zoezi hili la krejesha kwenye jamii zaidi ya mara mbili ili kutoa shukrani na kutambua kuwa umuhimu wa jamii kwao, kwani bila wao ni ngumu sana kufanya biashara.
Zoezi hili ni sehemu ya mpango endelevu wa CSR wa Meridianbet unaolenga kuboresha ustawi wa jamii kwa kugusa makundi mbalimbali yenye uhitaji kama shule, vituo vya afya, na familia zenye changamoto za kiuchumi.