::::::::
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Babyilon Mwakyambile ameingia kwenye mbio za ubunge kwa kuomba ridhaa kuteuliwa kugombea Jimbo la Kyela.
Mwakyambile ambaye kitaaluma ni mthaminiwa ardhi akiwa mhitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar Es Salaam, amesema ameamua kujitokeza kuwania nafasi hiyo ili kutimiza azma yake ya kuwatumikia wananchi kupitia jimbo hilo.