SABABU ZA KANYASU KUTIA NIA TENA, GEITA MJINI, FAIDA YA USOMI WANGU NI KUCHOCHEA MAENDELEO YA GEITA

:::::::::

MBUNGE anayemaliza muda wake, Geita Mjini, Costantine Kanyasu, ambaye aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, amechukua fomu ya kutetea nafasi yake hiyo, kuchochea maendeleo ya utekelezaji wa miradi iliyoanza katika uongozi wake.

Mbunge Kanyasu amekabidhiwa fomu hiyo, wilayani humo na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Geita, Michael Mshuya, huku akimshukuru Rais Dk.Samia kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuidhinisha fedha za utekelezaji miradi ya maendeleo ambayo alikuwa akiisemea mara kwa mara Bungeni.

Tangu Kanyasu kuingia katika Jimbo hilo, amefanya kazi kubwa ikiwemo kuchochea miradi ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya barabara, biashara, kuboresha huduma za jamii ikiwemo sekta ya afya, maji, jambo lililowezesha Mji huo kupandishwa kuwa Manispaa, hakika Geita ya sasa uwezi ilinganisha na miaka mitano au kumi ya nyuma.

Amechochea maendeleo ya Geita Mjini, kuwezesha kufanyika Maonesho ya kitaifa ya Madini, jambo ambalo limechochea ukuaji wa mji huo na kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wengi zaidi na kukuza mji huo kiuchumi.

Amesaidia ukuaji kisiasa wa Geita Mjini, kwani kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, wanasiasa wengi na wawekezaji wa Geita wametamani na kujitokeza kutia nia mwaka huu, wakifurahia maendeleo yaliyopo. Kwa ukomavu wake wa kisiasa Kanyasu amewapongeza watia nia hao akitamani wajitokeze wengi zaidi kwani amechochea maendeleo wanayotamani wengine.

Kanyasu ni hodari na mbobevu kisiasa kwani ni vigumu kumkuta katika migogoro ya kisiasa au kijamii ndani na nje ya Jimbo, bali amekuwa na ushirikiano mzuri na viongozi wa Chama na Serikali jimboni na kudumisha umoja na viongozi wa kitaifa wa Chama na serikali mara kwa mara wanaofanya ziara Geita Mjini.

Amesaidia vijana, wanawake na makundi maalumu kupata mitaji ya biashara kwa fedha zake binafsi na zile zinazotolewa na serikali kupitia Halmashauri ambayo hutolewa na serikali bila riba.

Katika huduma za Jamii, Kanyasu amewezesha vijiji vyote kufikiwa na umeme, wananchi kupata maji safi, ametetea wananchi waliokuwa na migogoro na wawekezaji wa uchimbaji madini, kupitia ziara zake Jimbo na kusikiliza kero za wananchi na kuwasilisha kwa viongozi husika ikiwemo Mawaziri.

Michango yake Bungeni ilijikita katika kutetea hoja wa wananchi hususan kulinda maslai ya wananchi wanaohamishwa kwasababu ya uwekezaji wa madini, kutafuta suluhu ya migogoro baina ya wachimbaji na wananchi, kutetea utekelezaji wa miradi ya kijamii na kiuchumi. Pia, amekuwa kipaumbele wa kutetea mijadala ya kitaifa yenye tija ya maendeleo ikiwa sehemu ya kumuunga mkono Rais Dk.Samia.

Kisiasa Kanyasu ni mbobevu na Mzalendo mwenye mizizi ya CCM aliyeanza safari yake ya kisiasa akiwa kijana akishika nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa vijana UVCCM, Geita.

Ana Elimu ya Shahada ya uzamili MBA, Astashahada ya Uongozi (PGD) Diploma in leadership, Degree ya Utawala wa Biashara BBA, Diploma ya Uvuvi – diploma in fish processing and marketing. Pia, amepitia JKT mwaka mmoja Bulombola operation vyama vingi. 

Kanyasu ni Mzaliwa wa Geita, alizaliwa Kalngalala, akasoma Nyankumbu na Geita Secondary, alifanya kazi Shirika la Kimataifa la Cahkula (FAO Kigoma, kushika nafasi ya Ukuu wa Wilaya , Mbunge na sasa ni Mkurugenzi wa Kampuni binafsi ya Global pharmaceuticals inayojihusisha na uagizaji, usambazaji wa dawa na vifaa Tiba.

Hakika huwezi kutaja Geita Mjini ya sasa, yenye mafanikio makubwa bila kumtaja Kanyasu, ni miaka kumi ya uwakilishi wenye mafanikio makubwa na mageuzi yaliyogeuza kuibadilli Geita, Kanyasu ametia nia kuendeleza safari anajua njia alizopita kuifikisha hapo, ameipandisha na kuipa heshima ya manispaaa katika Mkoa wa Geita. Geita Mjini ya sasa ya kisasa yenye utajiri inahitaji msomi wa aina yake wa kuifikisha kwenye kusudio.

 

Related Posts