Kifimbo cha Mfalme kutua nchini siku nne
KIFIMBO cha Mfalme kuashiria kuanza kwa msimu mpya wa michezo ya Jumuiya ya Madola, kitakimbizwa hapa nchini kwa siku nne kuanzia Agosti 2 hadi 6, 2025. Mbali na kukimbizwa, pia kifimbo hicho ambacho zamani kilifahamika kwa jina la kifimbo cha Malkia, kitachorwa vivutio vya Tanzania na kutangazwa kwenye michezo ijayo ya Madola itakayofanyika Glasgow, Scotland….