NeST yatajwa kuleta matunda, Serikali yatoa maagizo
Arusha. Matumizi ya mfumo mpya wa kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST), yametajwa kuongeza uwazi, uwajibikaji na kuleta thamani ya fedha katika manunuzi pamoja na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa. Mafanikio mengine yaliyochangiwa na mfumo huo yanatajwa kuwa ni pamoja na uboreshaji wa mazingira na kupungua kwa gharama za kufanya manunuzi kwa wazabuni na Serikali….