June 2025
π¦ππ₯πππππ ππ‘ππ§πππ ππ‘π π ππππ‘ππ’ πͺπ πͺππππ π¨
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Walimu katika elimu na malezi ya watoto katika nyanja mbalimbali za maisha. Waziri Mkenda amesema hayo Juni 14, 2025 jijini Dar es Salaam katika Hafla ya Utoaji wa Zawadi kwa Washindi wa Shindano la Tatu la Stadi za Ufundishaji kwa…
RAIS SAMIA NA RAIS WA BENKI YA AFRIKA AfDB WAKAGUA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE MSALATO
Muonekano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025. ujenzi wa Kiwanja hicho cha Msalato unahusisha njia ya kuruka na kutua ndege (runway) jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege pamoja na Miundombinu mengine. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi…
Matibabu ya saratani yazidi kuwa mzigo, Bugando yasaka Sh1 bilioni kusaidia wagonjwa
Mwanza. Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando imesema kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa saratani wanaohitaji matibabu lakini wanashindwa kumudu gharama. Hali hiyo imeweka hospitali katika mazingira ya kutoa misamaha mara kwa mara kwa wagonjwa hao, ili kuhakikisha wanapata huduma stahiki. Katika jitihada za kutafuta suluhisho la kudumu la changamoto hiyo, Hospitali ya Bugando imeanzisha…
Maeneo ya kipaumbele ya programu ya kizazi chenye usawa yatajwa
Dodoma. Wakati Programu ya Kizazi chenye Usawa (GEF), ikiendelea kutekelezwa nchini, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi MalumuΒ imetaja maeneo manne yaliyopewa kipaumbele ikiwamo kazi zenye staha kwa wanawake katika sekta isiyo rasmi. Maeneo mengine ni uwezeshaji wa kijinsia kwenye sekta binafsi, upatikanaji wa rasilimali za uzalishaji kwa wanawake na ubunifu na…
Mapigano Israel, Iran yazidi kuitikisa Mashariki ya Kati
Tehran, Iran.Β Hali ya wasiwasi imetanda Mashariki ya Kati baada ya mfululizo wa mashambulizi ya anga na makombora kati ya Israel na Iran, katika kinachoonekana kuwa moja ya machafuko makubwa zaidi ya kijeshi kwa siku za karibuni. Kwa mujibu wa magazeti ya The Telegraph la Uingereza na ‘The Wall Street Journal’ la Marekani, Iran imerusha makombora…
WMA YAFIKIA ASILIMIA 96 UTEKELEZAJI MPANGO KAZI WA MWAKA
Kibaha, Pwani Wakala wa Vipimo (WMA) umetekeleza Mpango Kazi wake wa Mwaka wa Fedha 2024/2025 kwa asilimia 96 ya malengo iliyojiwekea, kufikia mwezi Mei mwaka huu. Hayo yalibainishwa Juni 13, 2025 na Mtaalamu wa Uchumi kutoka Kitengo cha Mipango cha WMA, Benjamin Nkwera wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa kipindi husika…
Mahakama ya Rufani yaamuru sheria ya haki za kiraia irekebishwe
Arusha/Dar. Mahakama ya Rufani imeelekeza ndani ya miezi 12 (mwaka mmoja) Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lirekebishe kwa kufuta vifungu vya 6 na 7 vya Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) ya mwaka 2020, ambavyo vilifanyia marekebisho kifungu cha nne cha Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu (Bradea)….
Namelok Sokoine awataka wana-CCM kujibu hoja mitandaoni
Arusha. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Namelok Sokoine, amewataka viongozi na wanachama wa CCM mkoani Arusha kuwa mstari wa mbele kujibu kwa hoja maudhui ya kejeli dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan yanayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Namelok amesema hayo leo Juni 14, 2025, jijini Arusha, wakati wa mapokezi ya…
Tahliso yapendekeza mageuzi ya malipo ya ada na masharti kwa wanafunzi wa veta
Dodoma. Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso), Geofrey Kiliba ameiomba Serikali kuweka utaratibu mpya wa kulipa ada mara mbili kwa muhula hali itakayosaidia wanafunzi Β kusajiliwa na kuendelea na masomo kwa urahisi. Kiliba ametoa maombi hayo leo Juni 14, 2025, wakati wa maadhimisho ya miaka 21 ya Tahliso, yaliyoongozwa…