Wabunge walia na utajiri kwa wageni, umasikini kwa wazawa
Dodoma. Wakati pato halisi la Taifa lilifikia Sh156.6 trilioni mwaka 2024 kutoka Sh148.5 trilioni mwaka uliotangulia, wabunge wameonyesha hofu juu ya hali ya kukua kwa uchumi wa Tanzania huku ukuaji huo ukiwa hauakisi moja kwa moja pato la Mtanzania mmoja. Katika mdahalo wa uchambuzi wa bajeti kwa wabunge uliowakutanisha wabunge na wataalam wa mipango leo…