Jinsi bajeti ya Sh6.9 trilioni itakavyotumika Zanzibar

Dar es Salaam. Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa mwaka wa fedha 2025/26, yenye thamani ya Sh6.9 trilioni, itatumika katika sekta mbalimbali ikiwemo maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge, wawakilishi, na madiwani unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025. Maeneo yaliyopewa kipaumbele katika bajeti hiyo ni utekelezaji wa maendeleo yenye dhima ya Serikali inayoendelea…

Read More

Mwalimu: Kuiacha CCM kupita bila kupingwa ni dhambi

Arusha. Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Salum Mwalimu amesema chama hicho kinatambua historia ya siasa za upinzani hazijawahi kuwa rahisi Afrika, lakini itakuwa dhambi kubwa kukiachia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupita bila kupingwa Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwaka huu. Akihutubia wananchi kwenye mwendelezo wa mikutano ya hadhara ya Chaumma For Change…

Read More

Wasira: Uhuru wa kutoa maoni si kutukana wengine

Songea. Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema kuwa uwepo wa demokrasia na uhuru wa kutoa maoni haupaswi kuchukuliwa kama ruhusa ya kuvunja sheria au kutenda mambo yanayokiuka misingi ya maadili na heshima katika jamii. Amesema kuwa uwepo wa maridhiano nchini hauwezi kuchukua nafasi ya sheria, na kwamba ni lazima sheria za nchi…

Read More

Kauli ya CCM kuhusu Askofu Gwajima kuwania ubunge

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, kimetoa kauli kuhusu Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima kama anaruhusiwa kugombea tena au lah! Kauli ya CCM imekuja wakati ambao Askofu Gwajima yupo kwenye wimbi zito baada ya kanisa lake kufutwa. CCM imesema kuwa anaruhusiwa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania…

Read More

Vyanzo vinane kuchangia bima kwa wote VVU/Ukimwi

Dar es Salaam. Serikali katika mwaka 2025/2026 imependekeza kuanzisha vyanzo vya mapato vinane kwa ajili ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na kugharimia bima ya afya kwa wote. Hatua hiyo inatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa Sh586 bilioni. Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Juni 12, 2025 na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba alipowasilisha…

Read More

Gwajima ruksa kuomba kugombea tena ubunge

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, kimetoa kauli kwamba Mbunge wa Kawe, Mchungaji Josephat Gwajima anaruhusiwa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania tena nafasi hiyo kupitia chama hicho. Chama hicho tayari kimeshatangaza tarehe rasmi ya kuanza uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi ya ubunge na udiwani ndani…

Read More

Bara kama Zanzibar, bima ya watalii ikibisha hodi

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amependekeza kufanyika kwa marekebisho kwenye Sheria ya Bima, Sura 394 ili kuanzisha bima ya usafiri kwa wageni wanaoingia hapa nchini kwa kiwango cha dola za Marekani 44 kama ilivyo kwa upande wa Zanzibar. Oktoba 1,2024 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia ofisi ya Rais, Fedha na Mipango…

Read More