Rais Samia kufanya ziara mikoani, Msumbiji na Comoro

Dodoma. Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara mikoa ya Simiyu na Mwanza pamoja na nchi za Msumbiji na Comoro. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Juni 11, 2025, Msigwa amesema akiwa mikoa hiyo, Rais Samia atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi. Amesema Juni…

Read More

Chaumma yakazia sera ya kuwaongoza walioshiba

Tabora. Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), kimesema kikiingia madarakani kitaboresha sera ya kilimo ili wananchi wafanye shughuli hizo kwa tija na wapate chakula cha kutosheleza milo mitatu kwa siku. Hatua hiyo inakwenda Sambamba na sera ya ubwabwa ya chama hicho ya kuwa na Taifa lenye watu walioshiba ambao wataweza kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Mwenyekiti…

Read More

WATENDAJI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA KATIKA MAJUKUMU YAO

…….,.,. MWENYEKITI Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kanda ya Iringa, Moses Ambindwile, amewataka wenyeviti wa mitaa na watendaji wa kata kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu na mipaka ya madaraka yao ili kuepuka migogoro ya kisheria inayoweza kuathiri nafasi zao za uongozi katika jamii wanayoongoza. Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi hao yaliyoandaliwa kwa…

Read More

Fundi wa danadana Hadhara afariki, azikwa usiku huu

FUNDI wa danadana, mwanadada Hadhara Charles ambaye mwili wake umekutwa umefia chumbani tangu siku tatu zilizopita unazikwa usiku huu nyumbani kwake Chanika jijini Dar es Salaam. Hadhara aliyejizolea umaarufu mkubwa enzi za uhai wake kwa kipaji cha kuuchezea mpira atakavyo, amekutwa amefariki dunia ndani akiwa peke yake. Mdogo wa Hadhara aliyejitambulisha kwa jina la Mama Raiyan…

Read More

Simulizi jinamizi la ajali kwa maeneo haya Mbeya

Mbeya. Wakati zikiripotiwa ajali zinazoua makumi ya watu katika Mlima Iwambi jijini Mbeya, wakazi wa Mtaa wa Ndejele uliopo eneo hilo, wamesimulia namna walivyochoka kuokota maiti za ajali mara kwa mara, huku wakiitaka Serikali kuchukua hatua. Wamesema eneo hilo limekuwa hatari kwa ajali za mara kwa mara zinazohusisha pikipiki, bajaji, hiace na magari ya abiria…

Read More

Kanuni za Bunge kuibana Serikali, wageni

Dodoma. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha marekebisho ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari 2023, likilenga kuboresha uwajibikaji na kuongeza ufanisi wa shughuli za kibunge. Miongoni mwa marekebisho hayo ni kuwalazimu mawaziri kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa maazimio ya Bunge yanayotokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu…

Read More