Vurugu zaibuka mkutano wa Chadema Igunga, mmoja mbaroni
Igunga. Kijana Lufigo Bundala, mkazi wa Kijiji cha Ibuta kilichopo Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa tuhuma za kuanzisha vurugu, kushambulia na kujeruhi watu katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) uliofanyika leo Jumanne Juni 10, 2025. Akizungumza na viongozi wa Chadema waliofika Kituo…